1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la usalama.

Mtullya, Abdu Said17 Aprili 2008

Marekani na Uingereza zataka ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Umoja wa Mataifa katika kulinda amani barani Afrika.

https://p.dw.com/p/DjLI
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lajadili ufanisi katika majukumu ya kulinda amani barani Afrika.Picha: AP


Marekani na Uingereza  zimefafanua hatua za kuleta  ufanisi katika majukumu ya kulinda amani barani Afrika. Akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja  wa Afrika na Umoja wa Mataifa, katika baraza la Usalama, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Zalmay Khalilzad amesema,majukumu ya  kulinda amani yanayotekelezwa na Umoja wa Mataifa barani Afrika yanapaswa kuwekewa malengo ya kufahamika, kuhusu muda na bajeti.

Mkutano  baina ya viongozi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa uliitishwa kujadili njia za kuimarisha  ushirikiano katika suala la usalama baina ya pande mbili hizo.

Mwenyekiti wa mkutano huo rais Thabo Mbeki wa  Afrika  Kusini  amesema ni muhimu kwa majukumu ya  kulinda amani barani  Afrika kuongezewa fedha.