1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza jipya la mawaziri lakhairishwa kutangazwa

6 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/Dco3

NAIROBI

Mpango wa kutangazwa baraza jipya la mawaziri katika serikali ya mseto nchini Kenya umekhairishwa hadi muda usiojulikana kufuatia hali ya kutoelewana kuhusu muundo wa baraza hilo.

Msemaji wa serikali Dkt Alfred Mutua amesema rais Mwai Kibaki ameitisha mkutano na kiongozi wa Upinzani Raila Odinga hii leo ili wakamilishe mashauriano kuhusiana na suala hilo.Serikali imepinga orodha ya kwanza ya mawaziri iliyotolewa ijumaa na chama cha ODM.Rais Kibaki na waziri mkuu mtarajiwa Raila Odinga walikubaliana kulitangaza baraza jipya la mawaziri hii leo ambalo lingeapishwa mwishoni mwa wiki ijayo.Hatua ya kukhairishwa kutangazwa kwa baraza hilo jipya la mawaziri ni kipigo kikubwa kwa mpango wa utekelezaji wa makuabaliano yaliyoafikiwa mwezi Februari chini ya Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ya kumaliza ghasia zilizoibuka kufuatia matokeo ya uchaguzi wa urais ambayo chama cha ODM kilidai yalifanyiwa udanganyifu.