1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barack Obama aongeza Umaarufu New-Hampshire

8 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Clju

NEW HAMPSHIRE

Wakaazi wa jimbo la New Hampshire nchini Marekani wanajitaarisha kupiga kura ya maoni katika uchaguzi wa awali kabla ya uchaguzi war ais.Katika uchunguzi wa maoni uliofanywa siku za hivi karibuni unaonyesha seneta wa jimbo la Illinois Barack Obama amepata umaarufu mkubwa wa asilimi 10 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Hillary Clinton katika jimbo hilo la New Hampshire.Kwenye uchaguzi wa awali wa jimbo la Iowa Barack Obama alipata ushindi mkubwa wiki iliyopita.Kwa upande wa chama cha Republican waliowekwa katika nafasi nzuri ya kushinda kinyang’anyiro cha kura ya maoni katika jimbo la New Hampshire ni John MacCain na Mitt Romney.