BAQOUBA;Mkuu wa polisi auawa katika shambulizi la kujitoa mhanga | Habari za Ulimwengu | DW | 25.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAQOUBA;Mkuu wa polisi auawa katika shambulizi la kujitoa mhanga

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga, amejilipua katika mkutano wa maridhiano kati ya washia na wasunni na kuwaua watu 15 akiwemo Mkuu wa Polisi wa jimbo la Baqouba na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.

Msemaji wa Polisi Meja Salah la Juram amesema kuwa mlengwa wa shambulizi hilo alikuwa gavana wa jimbo hilo Raad Rashid ambaye alijeruhiwa huku dereva wake akiuawa.

Mkutano huo ulikuwa ukifanyika katika msikiti mmoja uliyoko kwenye mji huo katika viongozi wa kishia na kisunni na uliandaliwa na Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com