1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANNU PAKISTAN.Wanajeshi wanne wauwawa kwenye shambulio la bomu

4 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlw

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameshambulia msafara wa jeshi kaskazini mwagharibi mwa Pakistan katika mji wa Bannu na kujiua mwenyewe pamoja na wanajeshi wasiopungua wanne.

Mtu huyo aliyekuwa ametega bomu ndani ya gari alivurumisha gari lake katika kituo cha kukagua magari wakati msafara wa wanajeshi ulipokuwa ukitokea kaskazini mwa jimbo la Wazirstan kwenda Bannu karibu na mpaka wa Afghanstan.

Inaaminika wanajeshi wengi wamejeruhiwa katika tukio hilo ingawa bado hakuna taarifa zaidi.