1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGKOK: Waranti watolewa Shinawatra akamatwe

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSz

Mahakama moja nchini Thailand imetoa waranti mwingine wa kukamatwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Thaksin Shinawatra na mkewe, kwa madai ya uvunjaji wa sheria za biashara.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya washukiwa hao kushindwa kufika mahakamani baada ya waranti wa kwanza.

Thaksin Shinawatra ambaye anapinga madai yote yanayomkabili, amekuwa akiishi mjini London, Uingereza kwa kujitakia mwenyewe, tangu alipoondolewa madarakani katika mapinduzi ya amani mnamo mwezi Septemba mwaka jana.

Shinawatra amesema hatarejea nchini Thailand mpaka baada ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu.