Bangkok: Wanamgambo wanaowania kujitenga waua watu nchini Thailand. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bangkok: Wanamgambo wanaowania kujitenga waua watu nchini Thailand.

Polisi nchini Thailand wamesema waasi wanaowania kujitenga katika eneo la kusini la nchi hiyo, wamewaua watu wawili na wakawajeruhi wengine kumi na moja kwenye shambulio la kulipiza kisasi kutokana na uvamizi wa hapo awali wa polisi katika eneo hilo.

Wakuu wa serikali walisema wanamgambo wa majimbo matatu ya kusini mwa nchi hiyo walishambulia mara kadha wakuu wa usalama waliokuwa wakishika doria katika sehemu mbalimbali.

Wanamgambo hao wametekeleza mashambulio hayo siku moja baada ya makabiliano kati yao na polisi yaliyosababisha mauaji ya wanamgambo watano wa Kiislamu katika jimbo la Yala.

Watu zaidi ya elfu mbili na mia tatu wameuawa tangu mwaka 2004 wakati wanamgambo wa eneo la kusini walipoanzisha vita vya kuwania kujitenga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com