Bangkok. Wanafunzi wauwawa kwa risasi Thailand. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bangkok. Wanafunzi wauwawa kwa risasi Thailand.

Kiasi wanafunzi wawili wameuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa katika shambulio la risasi katika shule moja ya Kiislamu kusini mwa Thailand. Polisi wa Thailand wamesema watu ambao hawakutambulika walishambulia shule ya Bamrungsart katika jimbo la Sonkhla usiku wakati wanafunzi wakiwa wamelala.

Wamesema kuwa viongozi watatu wa dini ya Budha walipigwa risasi baadaye katika wilaya hiyo.

Kiasi cha watu 2,000 wameuwawa katika muda wa miaka mitatu iliyopita katika ghasia za harakati za kutaka kujitenga kwa jimbo hilo ambalo linaishi wafuasi wengi wa dini ya Kiislamu kusini mwa Thailand. Wiki iliyopita , Mabudha watatu waliuwawa katika shambulio la kushtukiza wakiwa katika basi dogo wakati wakisafiri kwenda kazini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com