BANGALORE : Anaendelea vizuri baada ya operesheni ngumu | Habari za Ulimwengu | DW | 10.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BANGALORE : Anaendelea vizuri baada ya operesheni ngumu

Msichana wa India mwenye umri wa miaka miwili ambaye amefanyiwa operesheni ngumu ya kumtenganisha na viungo vya ziada kwenye mwili wake hali yake inaendelea kuwa nzuri baada ya kupata fahamu kufuatia operesheni hiyo.

Lakshmi Tatma ambaye amezaliwa akiwa na mikono minne na miguu minne alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Sparsh kusini mwa mji wa Bangalore nchini India ambapo timu ya madaktari ilimfanyia opresheni hiyo iliodumu masaa 27.

Msichana huyo ambaye alikuwa hawezi kusimama wala kutembea alipata fahamu zake hapo jana kwa kufunguwa macho na kutabasamu na mama yake.

Hiyo ni operesheni ya kwanza ya aina yake kufanyika nchini India.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com