1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki-moon ataka hatua kali dhidi ya Assad

Sekione Kitojo15 Desemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameyataka mataifa yenye nguvu duniani kuchukua hatua kwa ajili ya ubinadamu dhidi ya ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Rais Bashar al-Assad.

https://p.dw.com/p/13TIx
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moonPicha: picture alliance ZUMA Press

Ban amezungumza mjini New York wakati alipolitumia baraza la usalama la umoja wa mataifa taarifa ya baraza la umoja wa mataifa la haki za binadamu ambayo inasema kuwa zaidi ya watu 5,000, ikiwa ni pamoja na raia na wanajeshi waliokimbia jeshi, wameuwawa tangu Machi mwaka huu. Hadi sasa, Urusi na China zimezuwia juhudi za mataifa ya magharibi kwa baraza hilo kutoa shutuma dhidi ya Syria.

Kundi la wanaharakati wa Syria wanaoangalia haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza limesema kuwa raia 21 wamepigwa risasi na kufariki na majeshi ya serikali nchini Syria jana, ikiwa ni pamoja na watu 11 katika mji wa Hama. Vikosi viliingia katika mji huo kuvunja mgomo wa siku tatu kwa ajili ya utu, ulioitishwa na upande wa upinzani. Serikali ya Syria imesema kuwa mzozo huo pia umesababisha wanajeshi 1,100 kuuwawa.