Bahrain yatunga sheeria kuhusu usafirishaji wa binadamu | Habari za Ulimwengu | DW | 09.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bahrain yatunga sheeria kuhusu usafirishaji wa binadamu

MANAMA:

Mfalme wa Bahrain-Hamad Bin Isa al-Khalifa, ametoa sheria ya kupambana dhidi ya kusafirisha binadamu.

Hatua hii imechukuliwa siku chache kabla ya ziara ya rais wa Marekani -George W.Bush.Marekani ambayo ina mkataba wa biashara huru na Bahrain,imekuwa ikizikosoa nchi zingine washirika wake katika Ghuba kwa kushindwa kuchukua hatua badhubuti za kuzuia bishara hiyo.Sheria inasema kuwa yeyote atakaepatikana na hatia atakwenda jela pamoja na kutozwa faini inayolingana na dola za kimarekani zaidi ya elf 5. Theluthi mbili ya wakazi wa kisiwa hicho ni wageni na imekuwa ikilaumiwa kwa kutowalinda vilivyo.Wengi wa wafanya kazi hao hutoka bara hindi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com