1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Watu zaidi ya 40 wauawa nchini Irak

16 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9R

Watu zaidi ya 40 wameuawa katika mashambulio kadhaa ya mabomu na kutokana na mashambulio ya kujitoa mhanga mjini Baghdad.

Polisi ya mji huo imesema kuwa watu 18 waliuliwa baada ya mabomu mawili yaliyotegwa ndani ya magari kulipuka sokoni katika sehemu ya mji huo inayokaliwa hasa na washia.

Watu wengine 11 walikufa baada ya basi dogo kulipuliwa katika mkoa wa karada wa mji huo. Shambilio hilo lilifuatiwa na jingine kaskazini mwa mji wa Baghdad ambapo watu sita waliangamia.

Habari zaidi kutoka Irak zinasema kuwa helikopta mbili za Uingereza zilianguka na marubani wake wawili wamekufa.Inatuhumiwa kuwa helikopta hizo ziligongana angani.

Na jeshi la Marekani limefahamisha kuwa askari wake watatu wameuawa.

Wakati huo huo watu walio karibu na kiongozi wa kidini wa washia bwana Moqtada al -Sadra wamesema kuwa kiongozi huyo anakusudia kuwaondoa mawaziri wake kutoka kwenye serikali ya mseto ya waziri mkuu Nouri al -Maliki.

Wabunge wamesema hatua hiyo ina lengo la kuishinikiza serikali ya bwana Maliki iandae ratiba juu ya kuondoka majeshi ya Marekani nchini Irak.