BAGHDAD.watu zaid ya 20 wameuwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 05.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD.watu zaid ya 20 wameuwawa

Milipuko mitatu ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari imesababisha vifo vya watu zaidi ya 20 na wengine wengi kujeruhiwa wakati watu waliokuwa na bunduki walipovamia maeneo mawili yanayokaliwa na Wasunni mashambulio hayo yametokea wakati jeshi la Marekani linajiandaa kutekeleza operesheni kubwa yenye lengo la kurudisha amani katika mji mkuu wa Baghdad nchini Irak.

Mshauri mkuu wa kikosi cha tisa cha jeshi la Irak amewaeleza waandishi wa habari kuwa zoezi hilo litaanza hii leo.

Kanali wa kimarekani Doug Heckman amesema operesheni kama hiyo haijawahi kutokea mjini Baghdad.

Katika operesheni hiyo wanajeshi wa Irak wakiongozwa na wanajeshi wa Marekani wataingia katika eneo moja hadi jingine mjini Baghdad kuwasaka wanamgambo na kuzitwaa silaha zisizo halali.

Operesheni hiyo inafuatia kuuwawa takriban watu 130 na kujeruhiwa watu wengine 300 mwishoni mwa wiki katika shambulio baya kuwahi kutokea tangu Marekani ilipo ivamia Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com