1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Watu kiasi cha 32 wuwawa kwa bomu nchini Iraq.

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxd

Bomu lililoripuka katika uwanja uliokuwa na watu wengi mjini Baghdad nchini Iraq leo asubuhi, limewauwa watu kiasi cha 32 na wengine 51 wamejeruhiwa.

Shambulio hilo limetokea katika maeneo ya Washia katika mji wa Sadr ambako wafanyakazi walikuwa wamejipanga wakisubiri kazi za kibarua.

Maeneo hayo ni ngome ya wanamgambo wa Mahdi ambao wanalalamikiwa kwa kusababisha maafa katika mji mkuu wa Iraq.

Aidha idadi ya vifo vya wanajeshi wa Marekani katika mwezi wa October imeongezeka na kufikia 100 na kuufanya mwezi huu kuwa ni mwezi unaoongoza kwa vifo kwa kipindi cha miaka miwili.

Wakati huo huo wakili mkuu anaemtetea rais wa zamani wa Iraq Sadam Hussein ametoka nje ya mahakama kwa hasira baada ya madai yake 12 kukataliwa.

Hata hivyo jaji mkuu amemteuwa mwanasheria mpya kumtetea Sadam Hussein ambae anashtakiwa kwa mauaji ya halaiki.