1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Watu 70 wauawa katika shambulizi la kisasi

Kiasi cha watu 70 wa madhehebu ya Sunni wameuawa katika mji wa Tal Afar kaskazini magharibi mwa Iraq, katika kile kinachoonekana kulipiza kisasi kutokana na shambulizi la mabomu hapo siku ya Jumanne lililowaua washia zaidi ya 55.

Msemaji wa jeshi la Iraq huko Mosul Luteni Kanali Mohamed Ahmed Salah amesema kuwa mauaji hayo yalitokea katika eneo la Al Wahda.

Naye Meya wa mji huo Brigadier Najim al Jubour amesema kuwa kundi la washia wenye silaha lilifanya mauaji hayo, ikiwa ni kulipiza kisasi cha mauaji ya hapo juzi.

Taarifa zinasema kuwa huenda watu hao walikuwa ni askari polisi wa kishia.Hali katika mji huo imekuwa tete kati ya wasunni, washia na wakazi wa kituruki.

Huko Faluja watu 15 wamejeruhiwa baada ya magari mawili kulipuka

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com