BAGHDAD:Watu 20 wameuwawa katika shambulio la bomu
28 Juni 2007Matangazo
Takriban watu 20 wameuwawa leo baada ya shambulio la bomu dhidi ya watu waliokuwa wamesimama kwenye kituo cha basi kusini magharibi mwa mji wa Baghdad nchini Irak.
Mabasi 40 yalilipuliwa katika mlipuko huo mkubwa.
Katika shambulio jingine kusini mwa Baghdad wanajeshi watatu wa Uingereza wameuwawa katika shambulio la bomu lililo tegwa kando ya barabra katika mji wa Basra, mwanajeshi wa nne amejeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.