1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Watu 11 wauwawa kwenye mashambulio ya mabomu

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6G

Watu wasiopungua 11 wameuwawa na zaidi ya wengine 50 wamejeruhiwa kufuatia mashambulio ya mabomu katika mji mkuu wa Iraq Baghdad.

Miripuko mitatu ya mambomu ilitokea nje ya soko lililoko kwenye eneo la kusini mwa mji wa Baghdad.

Waziri anayeshughulika na masuala ya viwanda nchini Iraq ambaye pia msafara wake ulikuwa ukipitia eneo hilo wakati mashambulio hayo yalipotokea ameponea chupuchupu shambulio hilo lakini walinzi wake watatu waliuwawa.