BAGHDAD:Wanajeshi wa Marekani wauawa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Wanajeshi wa Marekani wauawa


Wanajeshi wawili wa Marekani wameuwawa na wanne
kujeruhiwa katika baada ya gari lao kushambuliwa kusini magahribi mwa mji mkuu wa Irak-Baghdad.
Shambulio hilo lilitokea wakati maelfu ya wanajeshi wakiwa katika harakati zenye lengo la kupambana na wapiganaji wapinznai katika mji huo mkuu wakiwemo
wapiganaji wa kundi la Al Qaeda. Hadi sasa wapiganaji wapatao 41 wameuwawa na silaha nyingi kukamatwa.
Maafisa wa marekani kwa upande mwengine wanasema raia watano wa Irak waliuwawa na sita kujeruhiwa, wakati
kombora la wapiganaji lilipoliharibu jengo moja katika wilaya ya Al Mansour mjini Baghdad.


Katika tukio jengine la kujitoa mhanga dhidi ya
makao makuu ya polisi mjini Suleiman Beg , kusini
mwa Kirkuk, mtu aliyekua ndani ya gari alijiripua na
kuwauwa watu wapatao 14.Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com