BAGHDAD:Wajumbe wa Iran waachiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 29.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Wajumbe wa Iran waachiwa

Majeshi ya Marekani yamevamia hoteli moja mjini Baghdad na kuwazuia kwa muda mfupi raia 7 wa Iran.Hatua hiyo inatokea baada ya Rais George W Bush wa Marekani kuamuru makamanda wa jeshi la Marekani nchini Iraq kupambana na wapiganaji wa Iran anaowalaumu kufadhili vitendo vya ugaidi.

Iran kwa upande wake inashikilia kuwa tukio hilo halikubaliki kwani waliokamatwa ni maafisa katika wizara ya nishati.Hata hivyo kulingana na mshauri wa habari wa Waziri Mkuu Nuri al Maliki bwana Yassin Majid,raia hao 7 wa Iran waliachiwa asubuhi ya leo.Hii ni mara ya pili kwa jeshi la marekani kufanya kitendo kama hicho dhidi ya raia wa Iran tangu mwanzoni mwa mwaka huu.Januari 11 raia 5 wa Iran waliofanya kazi mjini Arbil walikamatwa na majeshi ya Marekani kwa madai ya kuwaunga mkono wanamgambo wanaopinga marekani.WaIran hao bado wanazuiliwa na MArekani mpaka sasa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com