BAGHDAD:Serikali yaelezea masikitiko yake juu ya vifo vya watu 15 | Habari za Ulimwengu | DW | 13.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Serikali yaelezea masikitiko yake juu ya vifo vya watu 15

Serikali ya Irak imeelezea masikitiko yake kufuatia vifo vya watu 15 katika shambulio la ndege za Kimarekani kwenye eneo linalo kaliwa na jamii ya Wasunni.

Watu hao kumi na tano walikuwa wanawake na watoto, serikali ya Irak imesema kuwa vifo vya raia haviwezi kuepukika katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Al Qaeda nchini humo.

Wakati huo huo watoto wawili wameuwawa na watoto wengine 17 wamejeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujilipua katika uwanja wa kuchezea kwenye mji wa Tuz kaskazini mwa Irak siku ya leo ya mapumziko kwa ajili ya Idd.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com