1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Sadri amshutumu Bush kwa kukataa kuondoa majeshi Iraq

28 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC69

Kiongozi wa kidini wa madhehebu ya shia nchini Iraq Muqtada al Sadri amemshutumu rais Bush wa Marekani kwa kukataa kuyaondoa majeshi yake Iraq.

Taarifa hiyo ya Sadri imesomwa mbele ya kikao cha bunge hii leo baada ya baraza la Congress la Marekani kuidhinisha mwsaada wa kutaka wanajeshi wake waondoke Iraq kufikia mwezi Okotoba tarehe mosi.

Al Sadri amesema kwenye taarifa hiyo kwamba ubishi wa rais Bush hautamfaidi chochote na ameshutumu pia matamshi ya kamanda wa juu wa jeshi la Marekani David Patreus na wenzake ambao wameonya ikiwa wataondoka Iraq kutakuwepo na machafuko zaidi.

Al Sadri ni kiongozi wa washia mwenye usemi mkubwa na inaaminika anaongoza makundi ambayo yanahusika na mauaji ya kimadhehebu ambayo yanaelekea kuitumbukiza Iraq kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.