1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Msikiti muhimu wa washia waripuliwa Sammarra

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBs5

Wanamgambo wameripua minara miwili ya msikiti muhimu wa madhehebu ya washia katika mji wa kaskazini wa Sammarra nchini Iraq.

Mripuko huo wa bomu uliolenga msikiti wa al Askari umefanywa na wanamgambo licha ya kuwepo vikosi vya usalama kwenye eneo hilo.

Mwaka jana wapiganaji wa kundi la mtandao wa Al Qaeda walifanya mashambulizi yaliyoharibu kabisa msikiti huo hali ambayo imesababisha mapambano makali ya kimadhehebu kati ya wasunni na washia kote nchini Iraq.

Serikali imetangaza hali ya kutotoka nje kwa muda usiojulikana.