BAGHDAD:Moto wazuka kwenye kituo cha jeshi la Marekani nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Moto wazuka kwenye kituo cha jeshi la Marekani nchini Irak

Moto uliozuka kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani mjini Baghdad ulisababisha miripuko kadhaa mikubwa.

Habari zinasema moto huo ulitokea kwenye bohari ya silaha, lakini hadi sasa hakuna habari iwapo umesababisha madhara yoyote.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Marekani,miripuko hiyo ilisababishwa na joto kali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com