1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.´Makamu wa rais anusurika katika shambulio la bomu

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOF

Watu 5 wameuwawa na watu wengine 25 wamejeruhiwa kufuatia mlipuko wa bomu katika jumba la wizara ya ujenzi mjini Baghdad ambamo makamu wa rais Adel Abdel-Mahdi alikuwa anahudhuria mkutano.

Makamu huyo wa rais amenusurika kifo lakini amepata majeraha kidogo na ametibiwa hospitalini.

Waziri wa ujenzi Riad Ghraib pia alipata majeraha madogo katika shambulio hilo.

Mlipuko huo ulitokea muda mfupi tu viongozi hao walipoingia katika chmba cha mkutano.

Abdel Mahdi anaefuata madhehebu ya Kishia ni mmoja kati makamu wawili wa rais wa Irak na ana nafasi kubwa ya kushikilia wadhfa wa urais iwapo rais Jalal Talabani mwenye umri wa miaka 74 anae uguwa hospitalini nchini Jordan atashindwa kuendelea kuongoza Irak au atafariki dunia.

Makamu mwingine war ais nchini irak ni Tarik Hashemi anaefuata madhehebu ya Kisunni.

Mji wa Baghdad pia ulikabiliwa na mfululizo wa mashambulio ya mabomu hapo jana siku ya jumapili.

Watu zaidi ya 50 waliuwawa.

Katika shambulio baya zaidi mshambuliaji wa kujitoa muhanga mwanamke alijilipua nje ya chuo cha elimu na kuwauwa watu 40 na kuwajeruhi watu wengine 35.