1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Mabomu yaendelea kuripuliwa nchini Iraq.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpz

Waasi wamewauwa kiasi cha watu 30 na kuwajeruhi wengine 95 hii leo katika mfululizo wa mabomu, ikiwemo mabomu matatu ya kutegwa katika gari.

Vyanzo vya habari vya kiusalama vimesema kuwa mashambulio hayo yametokea kwenye kitongoji cha wa-Shia huko Sadr City.

Gari moja yenye bomu iliripuka kwenye soko la Sadr City, mahala panapolengwa sana na waasi wa Kissuni katika ugomvi huu wa Iraq uliogharimu maisha ya maelfu ya Wairaq.