1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:11 wauwawa Iraq

Watu 11 wameuwawa magharibi mwa Iraq katika mji wa Karmah baada ya wapiganaji kuwakusanya watu hao ndani ya nyumba moja na kuiripua.Jeshi la Marekani linasema hatua hiyo huenda imechukuliwa na wapiganaji kulipiza kisasi dhidi ya wakaazi wa eneo hilo wanaunga mkono wanajeshi.

Tukio hilo limefanyika kwenye mkoa wa Anbar unaokaliwa na idadi kubwa ya wasunni ambako pia ni ngome ya wasunni wanaopinga uvamizi wa Marekani tangu kuangushwa utawala wa Saddam Hussein mwaka 2003.

Kwengineko nchini humo wizara ya mambo ya ndani imearifu kuwa vikosi vya usalama vya Iraq vimekamata mikanda 200 ya mabomu ya kujitoa muhanga na miripuko mingine ndani ya lori moja lililoingia Iraq kutoka Syria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com