1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Zaidi ya watu 30 wauwawa

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtB

Zaidi ya watu 30 wameuwawa nchini Iraq hapo jana.

Shambulio baya kabisa limetokea kusini mwa Baghdad ambapo mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha amejiripua na gari la mafuta na kuuwa wanajeshi 12 wa Iraq katika kituo cha ukaguzi wa kijeshi.

Na kaskazini mwa Iraq shambulio linaloonekana kuwa la roketi kwa gereza la Camp Bucca linaloongozwa na Marekani limeuwa takriban mahabusu sita na kujeruhi wengine zaidi ya 50.