1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Zaidi ya watu 122 wauwawa katika mashambulizi

Nchini Iraq zaidi ya watu 120 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi kadhaa ya kujitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa.

Katika wilaya inaokaliwa na wakaazi wengi wa madhehebu ya Washia mjini Baghdad watu zaidi ya 60 wameuwawa katika soko. Na karibu wakati huo huo magari matatu yaliotegwa mabomu yaliripuka katika mji mwengine unaokaliwa na Washia wengi wa Khalis kaskazini tu mwa Baghdad na kuuwa watu zaidi ya 40.

Mashambulizi hayo yanafuatia miripuko miwili ya mabomu katika eneo la Washia la Tal Afar hapo Jumanne ambalo limeuwa watu 85 na kuchochea shambulio la kulipiza kisasi la wapiganaji wa Kishia ambao wamewauwa Wasunni 70.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com