1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Watu watekwa nyara nchini Irak

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrv

Msafara wa magari ya raia, umesimamishwa na kundi la watu waliokuwa na silaha kusini mwa Irak na watu 14 wametekwa nyara. Wamarekani wanne ni miongoni mwa mateka hao.

Tukio hilo limetokea katika kituo cha ukaguzi wa abiria karibu na mji wa Nasiriyah.

Wakati hayo yakiarifiwa, waziri wa elimu wa juu wa Irak, Abd Dhiab, amesema watekaji nyara waliokamata na kushikilia kama mahabusu ma 10 ya watu kwenye jengo la serikali katika mji mkuu Baghdad, waliwatesa na kuwauwa baadhi ya mahabusu. Amesema hadi sasa watu kiasi ya 70 hawajulikani waliko.

Tamko hilo la waziri wa elimu ya juu limetofautiana na lile la waziri mkuu Nuri al-Maliki ambae alisema kuwa mateka wote 40 waliachiliwa huru.