BAGHDAD: Watu wanne wauwawa katika shambulio la bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 21.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu wanne wauwawa katika shambulio la bomu

Watu wanne wameuwawa wakati mshambuliaji wa kujitoa muhanga maisha alipojilipua ndani ya basi lililokuwa limewabeba abiria kutoka soko kubwa la Shorja mjini Baghdad. Watu 15 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Wengi wao walikuwa watoto na wanawake walioukuwa wametoka madukani kununua vitu vya kujiandaa na sikukuu ya kuadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Shambulio hilo limefanywa kufuatia mkutano wa mashehe wa madhebu ya Shia na Sunni nchini Irak mjini Mecca Saudi Arabia, ambako walisaini makubaliano ya kupiga marufuku machafuko na umwagaji damu kati ya makundi hayo mawili ya kiislamu nchini Irak.

Mkutano wa mjini Mecca umefanyika sambamba na siku ya mwisho ya sala ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wajumbe waliomuwakilisha waziri mkuu wa Irak, Nouri al Maliki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com