BAGHDAD: Watu takriban 18 wauwawa nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 11.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu takriban 18 wauwawa nchini Irak

Watu takriban 18 wameuwawa kwenye mapigano makali kati ya wanamgambo wa zamani wa kisunni na wanachama wa kundi la al Qaeda nchini Irak. Wanamgambo 16 wametekwa.

Wapiganaji wa kundi la Islamic Army nchini Irak walifanya shambulizi la kushangaza Ijumaa mchana karibu na Samara, kaskazini mwa mji mkuu Baghdad, na kutoa onyo kwa polisi wa Irak na jeshi la Marekani lisipeleke helikopta zake katika eneo hilo.

Idadi kubwa ya wanachama wa Islamic Army imejiunga na vita dhidi ya Al Qaeda vinavyoongozwa na Marekani, pamoja na wasunni na wapiganaji wengine wa zamani waliolikimbia kundi hilo kwa vitendo vyake vya kinyama na itikadi kali ya kidini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com