1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu 36 wauwawa

Vyombo vya habari nchini Irak vimeripoti kuwa watu kiasi ya 36 wameuwawa kwenye uvamizi wa usiku kucha uliofanywa na vikosi vya Uingereza na Irak kusini mwa mji mkuu, Baghdad.

Chombo kimoja cha habari nchini humo kimeitaja idadi ya watu waliouwawa kuwa 16.

Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu idadi ya raia waliouwawa kwenye operesheni hiyo.

Maafisa wa polisi nchini Irak wanasema wameshirikiana na wanajeshi wa Uingereza kupambana na jeshi la Mahdi linaloongozwa na shehe wa kishia, Moqtada al Sadr, katika mji wa Amara.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com