BAGHDAD: Watu 12 wauwawa kwenye mripuko wa bomu | Habari za Ulimwengu | DW | 02.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Watu 12 wauwawa kwenye mripuko wa bomu

Watu wasiopungua 12 wameuwawa leo katika mji wa Kirkuk kaskazini mwa Irak wakati mtu wa kujitoa mhanga maisha amejiruipua alipokuwa ndani ya lori. Miongoni mwa waliouwawa ni mtoto mchanga.

Mripuko huo ulitokea karibu na shule ya msingi na kituo cha polisi na majeruhi wengi miongi mwa watu watu 200 waliojeruhiwa walikuwa wanafunzi.

Duru za polisi zinasema shambulio hilo mlimefanyakika sambamba na ziara ya vikosi vya jeshi la Markani katikakituo hicho cha polisi ambacho ni makao makuu ya idara ya ukachero mjini Kirkuk.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com