1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanamgambo wanaimarisha mashambulizi Irak

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPH

Watu wasiopungua 15 wameuawa Jumapili katika mapigano na mashambulizi ya bomu,nchini Irak. Tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani,idadi ya vifo vilivyosababishwa na machafuko,imefikia 44.Kundi la “Islamic State of Iraq“ lenye uhusiano na Al-Qaeda limeonya kuwa litafanya mashambulio mapya wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhan.Vile vile kundi hilo limeonya kuwa litawalenga viongozi wa Kisunni wanaounga mkono vikosi vya Kimarekani nchini Irak.