Baghdad. Wanajeshi wa Marekani wauwawa. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Wanajeshi wa Marekani wauwawa.

Wanajeshi watatu wa Marekani wameuwawa wakati mlipuko ulipotokea karibu na magari yao ya doria katika jimbo la kaskazini la Diyala nchini Iraq.

Jeshi la Marekani limeripoti kuwa wanajeshi wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo na wamesafirishwa kwenda katika vituo vya kutoa matibabu vya jeshi hilo.

Jimbo la Diyala limeelezwa na rais wa Marekani George Bush siku ya Jumamosi kuwa ni sehemu ambayo inakabiliwa na mapambano dhidi ya watu wenye imani kali. Wakati huo huo , serikali ya Iraq imesema kuwa itaangalia upya hali ya makampuni ya usalama yanayofanyakazi nchini humo baada ya tukio la kurushiana risasi lililowahusisha walinzi kutoka kampuni la ulinzi la Marekani la Blackwater. Wizara ya mambo ya ndani imesitisha liseni ya kampuni la Blackwater baada ya mapigano hayo mjini Baghdad na kusababisha kiasi raia wanane kuuwawa siku ya Jumapili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com