BAGHDAD: Wanajeshi sita wa Marekani wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 31.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Wanajeshi sita wa Marekani wauwawa

Jeshi la Marekani nchini Irak limetangaza kwamba wanajeshi wake sita wameuwawa mjini Baghdad na vitongoji vyake. Idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouwawa katika mwezi huu wa Disemba nchini Irak sasa imefikia 109.

Idadi hiyo ni zaidi ya mara tatu ya wanajeshi waliouwawa mwezi Oktoba. Kwa jumla wanajeshi 2998 wa Marekani wameuwawa tangu uvamizi wa Irak mnamo mwaka wa 2003.

Rais George W Bush wa Marekani anatarajiwa kutangaza mpango mpya wa Marekani kuhusu Irak mwaka ujao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com