1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wairaq kadha wakimbia nchi yao kila mwezi.

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3A

Shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi limesema kuwa zaidi ya watu 40,000 kila mwezi wanaikimbia Iraq na zaidi ya watu 1.5 milioni wanakimbia makaazi yao nchini humo binafsi.

Msemaji wa shirika hilo la umoja wa mataifa amesema kuwa mamia kwa maelfu ya wairaq wanahamia nchini Uturuki, Lebanon, Misr na mataifa ya ghuba pamoja na Ulaya. Amesema kuwa Wairaq hivi sasa ni kundi kubwa kabisa la watu wanaotafuta hifadhi katika mataifa ya ulaya.

Ameeleza kuhusu ghasia za kimadhehebu na idadi kubwa ya watu wanaouwawa kuwa sababu zinazosababisha uhamaji huo.