BAGHDAD: Wafanyakazi wa shirika la hilali nyekundu waachiliwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 19.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Wafanyakazi wa shirika la hilali nyekundu waachiliwa huru

Watekaji nyara wamewaachilia huru wafanyakazi 26 kati ya wafanyakazi 30 wa shirika la hilali nyekundu mjini Baghdad. Wafanyakazi hao walitekwa nyara siku mbili zilizopita mjini Baghdad.

Msemaji wa shirika la hilali nyekundu amesema anatarajia kwamba wafanyakazi wengine waliosalia wataachiliwa huru wakati wowote.

Watu waliokuwa na bunduki walizivamia ofisi za shirika la hilali nyekundu mjini Baghdad mnamo Jumapili iliyopita na kuwateka nyara wafanyakazi wa kiumue wakidai walikuwa wakifanya uchunguzi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com