1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Umwagaji wa damu unaendelea Irak

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPO

Shambulizi la kujitolea maisha muhanga limeua watu 6 na kujeruhi 18 wengine,nje ya mkahawa katika mji wa Tuz Khurmato,kaskazini mwa Irak. Mshambulizi alievaa mkanda uliopachikwa miripuko alijiripua kwenye mkahawa huo.

Shambulizi hilo limetokea siku moja baada ya kundi la “Islamic State in Iraq“ linaloongozwa na Al-Qaeda kutangaza msimu mpya wa mashambulizi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Siku ya Jumamosi,shambulizi lililofanywa kusini-magharibi ya mji mkuu Baghdad,liliuwa watu 10 na wengine 15 walijeruhiwa.Wengi wao walikuwa wakipiga foleni kununua chakula kwa ajili ya futari yao.