BAGHDAD: Umwagaji damu unaendelea nchini Iraq
16 Mei 2007Matangazo
Machafuko yanaendelea nchini Iraq.Lori lililopakia gesi ya klorini liliripuliwa sokoni katika mji wa Abu Sayda,kaskazini mwa Baghdad eneo ambako Washia wengi huishi.Si chini ya watu 45 waliuawa na wengine 60 wamejeruhiwa.Kwa upande mwingine katika mji wa Nasriya watu 8 waliuawa na 40 walijeruhiwa baada ya vikosi vya Kiiraqi kupambana na wanamgambo wanaomuunga mkono Shehe wa Kishia,Moqtada al-Sadr.Shambulio hilo lilitokea baada ya polisi kuwakamata wanamgambo 2 siku ya Jumanne,wakishukiwa kuhusika na kundi linalofukia mabomu katika ukingo wa barabara.