BAGHDAD : Shambulio lauwa 35 | Habari za Ulimwengu | DW | 07.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Shambulio lauwa 35

Nchini Iraq takriban watu 35 wameuwawa katika shambulio la kujitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa katika gari la mizigo.

Wengi waliopoteza maisha yao inasemekana kuwa ni wanawake na watoto.Polisi imesema gari hilo lilirupuliwa na dereva wake katika mji wa Ramadi ulioko kama kilomita 110 magharibi mwa mji mkuu wa Baghdad.

Takriban watu 40 wamejeruhiwa kwenye mripuko huo ambao umetowa gesi ya chlorine hewani.

Ramadi ni mji mkuu wa jimbo la Anbar ambalo ni ngome kuu ya waasi wa Kiarabu wa madhehebu ya Sunni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com