BAGHDAD: Shambulio la bomu limeua watu 17 | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Shambulio la bomu limeua watu 17

Watu 17 wameuawa na wengine 25 wamejeruhiwa, katika shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari mjini Baghdad.Kwa mujibu wa polisi,watoto wengi ni miongoni mwa wale waliouawa na kujeruhiwa baada ya gari hilo kuripuliwa karibu na kundi la wageni waliokwenda kusherehekea harusi katika mtaa wa Abu Dshir ambako wengi wanaoishi ni wa madhehebu ya Kishia.Wakati huo huo vikosi vya Marekani na Iraq vimezindua operesheni kuu ya kijeshi ndani na ukingoni mwa Baghdad,katika juhudi ya kukomesha umwagaji damu kati ya makundi ya Kishia na Kisunni.Masoko na njia zimefungwa na idadi ya vituo vya ukaguzi imeongezwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com