1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Saddam huenda akanyongwa wakati wowote.

30 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCf2

Afisa mwandamizi wa Iraq amesema kuwa rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein atanyongwa kabla ya alfajiri leo Jumamosi mjini Baghdad.

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki amesema hakutakuwa na uchelewesho katika hukumu hiyo.

Wakati huo huo shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa mawakili wa Saddam Hussein wamemtaka jaji wa Marekani kuzuwia mteja wao kukabidhiwa kwa maafisa wa Iraq ambao wanasubiri kutekeleza hukumu ya kifo.

Mawakili wa Saddam wamesema tayari amekwisha hamishwa kutoka katika kituo cha jeshi la Marekani, licha ya kuwa wizara ya ulinzi ya Marekani imekanusha taarifa hizo.

Mwezi uliopita dikteta huyo wa zamani alihukumiwa kifo kwa kuhusika kwake na mauaji ya mwaka 1982 ya watu zaidi ya 150 katika mji wa Washia wa Dujail.