Baghdad. Polisi wanane wauwawa. | Habari za Ulimwengu | DW | 27.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Polisi wanane wauwawa.

Shambulio dhidi ya mlolongo wa magari ya polisi kaskazini mwa mji wa Baghdad limesababisha kuuwawa kwa polisi wanane, ikiwa ni pamoja na kamanda mmoja.

Shambulio hilo lilitokea katika mji wenye ghasia wa Baquba, kilometa 60 kaskazini ya Baghdad.

Mapema jana Alhamis , watu wenye silaha wameshambulia kituo kimoja cha polisi maalum wa Iraq katika mji mwingine karibu na Baquba, na kuuwa polisi sita na kuwajeruhi wengine 10.

Baquba ni ngome kuu ya wapiganaji wa Kisunni wanaopambana na majeshi ya Marekani pamoja na serikali inayoongozwa na Washia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com