Baghdad. Mshambuliaji wa kujitoa muhanga auwa watu 11. | Habari za Ulimwengu | DW | 30.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baghdad. Mshambuliaji wa kujitoa muhanga auwa watu 11.

Mtu aliyejitoa muhanga ameshambulia msikiti wa Washia katika mji wa Khalis kaskazini ya Baghdad. Polisi wa Iraq wamesema kuwa kiasi watu kumi wameuwawa na wengine 11 wamejeruhiwa.

Mshambuliaji huyo alilipua bomu hilo alilokuwa amelivaa muda mfupi baada ya sala ya Ijumaa.

Katika mji wa Kut, kusini mwa Baghdad, polisi mmoja wa Iraq ameuwawa na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya katika shambulio la kombora katika makao makuu ya kikosi cha kushambulia kwa ghafla.

Kikosi hicho kiko pamoja na majeshi ya Marekani. Mwanajeshi mmoja wa Uingereza ameuwawa baada ya bomu lililotegwa kando ya barabara kulipuka katika mji wa Basra kusini ya Iraq. Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kuwa mwanajeshi huyo alikuwa katika doria wakati bomu hilo lilipolipuka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com