1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Mripuko wa pikipiki sokoni waua watu mjini Baghdad, Iraq.

Kiasi watu wanne wamefariki na wengine ishirini wamejeruhiwa kwenye mripuko wa bomu mjini Baghdad.

Polisi wamesema maafa hayo yalisababishwa na pikipiki iliyoripuka sokoni katikati ya mji huo mkuu wa Iraq.

Wakati huo huo, ubalozi wa Marekani umethibitisha raia watano Wamarekani wafanyikazi wa kampuni ya ulinzi ya kibinafsi wameuawa.

Watu hao waliuawa siku ya jumanne iliyopita walipokuwa wakiwalinda wafanyikazi wa ubalozi huo waliokuwa kwenye mkutano wao wa kawaida.

Walinzi wanne miongoni mwao walifariki baada ya helikopta iliyokuwa ikishika doria hewani karibu na ubalozi kutunguliwa.

Makundi mawili ya wanamgambo wa kisunni yamekiri kuhusika na shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com