BAGHDAD: Mripuko wa bomu Iraq umeua watu 25
22 Mei 2007Matangazo
Hadi watu 25 wameuawa na kama 60 wengine wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea mji mkuu wa Iraq,Baghdad.Watoto wengi ni miongoni mwa wahanga wa shambulizi hilo.Kwa mujibu wa polisi, bomu lililotegwa ndani ya gari liliripuliwa katika soko lililojaa watu katika mtaa wa Amil mjini Baghdad,ambako wakazi wengi ni wa madhehebu ya Kishia.