BAGHDAD: Mmuagiko wa damu umezidi Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 02.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Mmuagiko wa damu umezidi Irak

Nchini Iraq raia waliouawa katika mwezi wa Oktoba imefikia idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa katika mwezi mmoja.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Irak,mwezi uliopita kama raia 1,300 waliuawa katika machafuko yaliochochewa kisiasa au kidini.Hiyo ni asili mia 20 zaidi kuliko mwezi wa Septemba.Mbali na idadi hiyo,wanajeshi na polisi 139 pia wameuawa katika ghasia zinazoendelea.Wachunguzi wa kimataifa lakini wanasema,idadi ya watu waliouawa ni kubwa zaidi. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,nchini Irak hivi karibuni zaidi ya watu 3,000 wamekuwa wakiuawa kila mwezi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com