1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mashambulio ya mabomu ya kujitoa mhanga yaendelea Iraq

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByk

Watu kiasi ishirini na watano wameuawa na wengine zaidi ya thelathini wamejeruhiwa baada ya shambulio la bomu la kutegwa ndani ya gari kwenye mazishi ya kiongozi mmoja wa kienyeji aliyeuawa mjini Fallujah, magharibi mwa Iraq.

Wakati huo huo, majeshi ya Marekani yamethibitisha maiti ilioopolewa kutoka mto wa Euphrates, kusini mwa Baghdad, ni ya mmoja miongoni mwa askari-jeshi watatu wa Marekani waliotoweka nchini Iraq.

Majeshi hayo yalianzisha msako mkali baada ya shambulio la tarehe kumi na mbili mwezi huu ambapo wanajeshi wanne na mkalimani wao waliuawa.

Kundi lijiitalo Taifa la Kiislamu la Iraq ambalo lina uhusiano na mtandao wa al-Qaeda lilikuwa limedai linawashikilia wanajeshi hao.

Wakati huo huo, maelfu ya wanajeshi ya Marekani wakishirikiana na askari wa Iraq, wameendelea na msako wao kuwatafuta askari wawili ambao hawajapatikana.