BAGHDAD: Mashambulio ya kujitolea muhanga yameua watu 60 | Habari za Ulimwengu | DW | 02.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Mashambulio ya kujitolea muhanga yameua watu 60

Nchini Irak,watu wasiopungua 60 wameuawa na kama 150 wengine wamejeruhiwa katika mashambulio mawili ya kujitolea muhanga.Mabomu mawili yaliripuka,moja baada ya jingine,kwenye soko lililojaa watu katika mji wa Hillah ambako wakaazi wengi ni wa madhehebu ya Kishia.Wakati huo huo katika mji mkuu Baghdad,mashambulio ya bomu na makombora,yameua si chini ya watu 11.Vile vile askari polisi mjini Baghdad wamesema wamegundua maiti za watu 30.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Irak,ghasia zinazoendelea nchini humo,zimeua takriban raia 2,000 katika mwezi wa Januari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com